MAMA SAMIA ATOA MILIONI 500 KWA KILA JIMBO

  

 


Home | Tanzania Rural and Urban Roads Agency-TARURA

KATIKA kufanikisha ujenzi wa barabara za ndani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ameidhinisha fedha kiasi cha shilingi milioni 500 kwa kila jimbo nchi nzima kwa ajili ya TARURA.

Akizungumza Bungeni jijini Dodoma Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu amesema;

 “Kwa mara ya kwanza, tumepata fedha Bilioni 172 kutoka mfuko mkuu wa hazina kwa sababu fedha hizi tumezipata haraka haraka na bajeti ilishapitishwa na Kamati, tumetumia maamuzi ya Jumla kila jimbo tunapeleka Milioni 500 kwa ajili ya TARURA ili Barabara zijengwe..

"Na hii ndiyo kazi Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amesikia kilio chenu,” alisema Waziri Ummy.

Hatua ya utengenezaji wa barabara katika kila jimbo ni muendelezo wa Rais Samia kutaka kila kona ya nchi inakua na barabara ya uhakika ambazo zitarahisisha ufanyikaji wa shughuli za kiuchumi.

 

No comments