GSM WAMKARIBISHA YUSSUF MANJI YANGA

  

Alichokisema Eng Hersi Said

MKURUGENZI wa Uwekezaji wa Kampuni ya GSM, Injiinia Hersi Said amesema wanamkaribisha kwa mikono miwili na moyo mweupe kabisa, mfanyabiashara maarufu Yussuf Manji kurejea Yanga.

Akihojiwa na kituo cha redio cha Efm cha Sports HQ, Hersi alisema kwa sasa kampuni hiyo inagharamikia kila kitu kwa sasa ndani ya klabu hiyo, ikiwa ni pamoja na mishahara kwa asilimia mia moja, kambi, usafiri, usajili na kadhalika.

"Akitokea mtu akaja akasema nyinyi GSM fanya hivi, mimi nitagharamia huku, tunamkaribisha kwa mikono miwili, lengo letu kubwa na la msingi ni kuhakikisha klabu hii inasonga mbele," alisema.

No comments