KWELI BABA LEVO CHAWA, MSIKIE AKIMSIFIA DIAMOND

DIWANI wa zamani wa ACT Wazalendo huko Kigoma ambaye pia ni msanii wa muziki wa kizazi kipya, Baba Levo, amethibitisha kuwa yeye ni chawa, neno linaloshabihiana na mpambe wa kutupwa wa Diamond Platnumz.
Akiwa mzima wa afya, amekiambia
kituo kimoja cha televisheni za mtandaoni kuwa Diamond ambaye ameteuliwa kuwania
Tuzo za BET mwaka huu, anajenga mjengo ambao kwa msanii wa kawaida nchi hii,
itamchukua kati ya miaka 30 hadi 40 kuimaliza!
"Ni uwekezaji wa nyumba yenye
thamani ya shilingi bilioni 800, hela ambazo anazo, anaweza kula kwa miaka 300
na hapo kila siku awe anakula milioni moja."

Post a Comment