HAMNIJUI NYINYI, MIMI COSTO WA KUTUPWA- KARIA

DUNIA nzima ya wapenzi na mashabiki wa soka Tanzania wakiamini kuwa Rais wa TFF, Wallace Karia ni shabiki wa kutupwa wa mabingwa wa nchi, Simba, mwenyewe ameona kukaa kimya kunam-cost, hivyo amejitokeza na kusema si kweli.
Karia ambaye amekuwa akishutumiwa waziwazi na mashabiki na viongozi wa Yanga juu ya hilo, amesema hana mahaba na Simba ila ishu kama ni kupenda timu, yeye ni mtu wa Coastal Union ya nyumbani kwao Tanga.
"Mimi kama ni mahaba ya timu yako Coatal Union na iko kubaya, inaishia shimoni, ila kusema nina mahaba na Simba inatoka wapi au naichukua Yanga kwa sababu gani.
"Mimi hata ugomvi na Yanga
sina, ni maneno ya watu tu, lakini katika maisha ukiwa kiongozi hauwezi
kumfurahisha kila mtu na sio kwamba utendaji wangu utamfurahisha kila mtu, kuna
mwingine nitamkera kutoka na utashi wake" amesema Karia.

Post a Comment