JOKATE FULL MAUJIKO WILAYANI KISARAWE

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo ambaye wakati
akiteuliwa kushika nafasi hiyo alipokewa kwa hisia tofauti, hivi sasa anapewa
sifa kama mmoja wa viongozi vijana wenye uwezo mkubwa wa kufanya kazi za
maendeleo.
Katika kipindi chake cha uongozi, mrembo huyo namba mbili
wa Miss Tanzania mwaka 2006, ameipaisha wilaya hiyo katika nyanja za elimu na
uchumi.
Kisarawe ni moja kati ya halmashauri tisa za mkoa wa Pwani
ikiwa imeanzishwa tarehe 1 Julai 1907. Wilaya ya Kisarawe inapakana na Wilaya
ya Mkuranga kwa upande wa Kusini-mashariki na Wilaya ya Morogoro upande wa
Magharibi. Mashariki-Kaskazini kuna Jiji la Dar es Salaam, Kaskazini Wilaya ya
Kibaha na Kusini Wilaya ya Rufiji. Lakini Utafikiri Kisarawe ndo Mkoa kumbe ni
Wilaya tu kati ya Wilaya 9.
Pamoja na kukuta watu wa Pwani ni wavivu, kwa muda mchache
aliokaa Kisarawe, ameitambulisha kimataifa. Kisarawe imekuwa Maarufu.
Baadhi
ya mambo ambayo ameyafanya na yanaonekana.
Elimu
Wanafunzi walikuwa watoro na Shule za Kisarawe zilikuwa
zinafanya vibaya, lakini sasa zinafanya vizuri.
Wilaya ya Kisarawe aliikuta ina uhitaji wa madawati 1166
ambapo kwa sekondari uhitaji ni 484, na 642
kwa shule ya msingi. Kafanyia kazi
Alikuta wilaya ina uhitaji wa shilingi milioni 124 kwa ajili
ya kujenga matundu ya vyoo 113 Mashuleni, kafanyia kazi
Alikuta Wilaya inauhitaji wa ofisi za walimu za kisasa
katika shule 14 ambazo zinagharimu shilingi milioni 880. Kafanyia kazi
Alikuta Wilaya haina Maktaba, zinajengwa.
Alikuta Kisarawe ina
matatizo ya Maji. Kwa muda mfupi tatizo la Maji limepungua.
Huduma za afya zimeboreka hasa huduma ya Mama na Mtoto.
Ujenzi wa Wodi ya Upasuaji.
Huduma ya Umeme imeboreka nk.
Ameweza kufanya mambo ya Maendeleo bila kuwasumbua vyama
pinzani wala kujenga chuki kwa wananchi. Hajihusishi na Ufusadi. Ana heshima
kwa Kila mtu na ni msikivu.
Jokate ni Mfano kwa Viongozi wanaoteuliwa sasa.

Post a Comment