HIZI NDIZO SABABU HASA ZA MANJI KUKAMATWA

HUKU kukiwa na maswali mengi mtaani juu ya nini hasa kinaendelea kati ya mfanyabiashara mkubwa nchini, Yussuf Mehboob Manji na dola, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ambayo ndiyo inamshikilia, imetoa taarifa zifuatazo.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Takukuru Kamishna wa Polisi Said
Hamduni, Manji anashikiliwa toka alipowasili nchini Tanzania akituhumiwa kwa
makosa yafuatayo;
1) Kukwepa kodi :
Kampuni zake za Intertrade Commercial LTD Service na Golden
Globe International Service Limited zinatuhumiwa kwa kutolipa kodi ya VAT kati
ya mwaka 2011 na 2015.
2) Udanganyifu
wakati wa manunuzi ya hisa za kampuni ya Tigo.
3) Kupitia
kampuni yake ya Quality Group kuna maswali kuhusu mapato ya klabu ya Yanga
ambayo alikuwa akiidhamini na kuiongoza kama mwenyekiti wakati huo.
4) Kuhujumu usalama wa taifa kwa kukutwa na vitambaa
vinavyotengeza sare za jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ vyenye thamani ya
zaidi ya shilingi milioni 200 za Kitanzania.
Manji aliondoka nje ya nchi mwaka wa 2018 baada ya Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam kumuachia huru pamoja na wenzie
watatu Septemba 2017 walipokuwa wakituhumiwa kwa makosa saba ya uhujumu uchumi.

Post a Comment