BOSSLADY ZARI ATINGA BUNGENI DODOMA

MWANAMAMA Zarina Hassan anayefahamika pia kama Zari The BossLady, ambaye ni maarufu hapa nchini kutokana na kuzaa watoto wawili na staa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz, yupo mjengoni akiwa mmoja wa waalikwa leo hii.
Zari amekaribishwa kushuhudia
shughuli za Bunge akiwa amealikwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dr. Damas
Ndumbaro. Zari kwa sasa ni Balozi wa Hiari wa Utalii Tanzania.
Zari alitua Airport Dar es salaam juzi akitokea South Africa
kwa ajili ya kazi zake za Ubalozi ikiwemo kugawa taulo za kike kwa wasichana
mbalimbali Dar es Salaam.

Post a Comment