GARI LA AKON LAREJESHWA, AMSAHEME MWIZI
SIKU chache zilizopita, iliripotiwa kuibiwa kwa gari la staa wa muziki mkubwa wa Marekani, Akon, inaelezwa kuwa gari hilo lilipatikana kutokana na kazi kubwa ya Polisi na alirejeshewa siku iliyofuata.
Kwa mujibu wa tovuti ya TheShadeRoom, aliwasilisha malalamiko yake
katika idara ya polisi ya Atlanta kwa kudai kuibiwa Gari hilo aina ya Range
Rover #SuV
Hata hivyo, polisi walifanya kila liwezekanalo hadi
kufanikiwa kulipata gari hilo na kumkabidhi Star huyo siku iliyofuata.
Kwa sasa Star huyo anaripotiwa kumsamehe mtuhumiwa huyo
aliyebeba gari lake kwa kile alichoeleza kuwa ni ugumu wa maisha ndiyo sababu
ya mtu huyo kufanya tukio kama hilo la kihalifu.
Pia @akon ameenda mbali
zaidi na kueleza kuwa hata yeye pia anaelewa maisha kwani kabla hajafanikiwa
alipitia kwenye misoto mingi hivyo hatohitaji malipo yoyote.

Post a Comment