34 WADAKWA WIZI WA KUKWAPUA SIMU, MIKOBA KWA BODABODA MORO

VIJANA wapatao 34 wamekamatwa na Jeshi
la Polisi mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za wizi wa kukwapua mali za wananchi kwa
kutumia pikipiki ambapo jumla ya pikipiki nane zinashikiliwa na jeshi hilo.
Kwa mujibu wa Fortunatus Musilimu ambaye ni RPC Morogoro,
vijana hao wamedakwa katika maeneo ya Mji Mpya, Mwembesonga, Kidabaga na
Mtawala.
Inadaiwa vijana hao hupakizana
wawili kwenye pikipiki hizo na kuvizia watembea kwa miguu wanaoongea na simu au
walioshika mikoba na kuikwapua.
Katika hatua nyingine SACP Musilimu, amesema jeshi hilo
linawashikilia watu watatu kwa tuhuma ya wizi wa vifaa vya ujenzi wa reli ya
kisasa ya SGR ikiwemo vipande vya nyaya za shaba mpya na zilizounguzwa huku
nyingine zikiwa zimefumuliwa kwenye 'transfomer' zenye jumla ya uzito wa
kilogramu77.9 zilizokuwa zimehifadhiwa katika ghala la mfanyabiashara
aliyefahamika kwa jina moja la Ahmed lililopo mtaa wa Modeco Manispaa ya Morogoro.

Post a Comment