RUKSA KUBEBA SILAHA NA KUJILINDA TEXAS

KATIKA kukabiliana na wimbi kubwa la mauaji yanayotokea kila siku jimboni Texas, wabunge wamepitisha muswada utakaoruhusu Wakazi wa Jimbo hilo kubeba bunduki na kutembea nazo mtaani hata kama hawana vibali vya kubeba silaha tofauti na sasa ambapo sheria inataka yeyote anayebeba bunduki kuwa na leseni, awe pia na mafunzo ya kuitumia lakini pia historia yake lazima ichunguzwe.
Wanaounga mkono sheria hiyo mpya wanasema itaruhusu Raia wa
Texas kujilinda wenyewe huko mitaani na huenda ikasaidia Raia kujibu
mashambulizi pale mtu mwenye silaha anapofyetua risasi bila sababu kwenye eneo
la umma kama ambavyo imetokea Watu kuua Watu kanisani, super market na sehemu
nyingine za umma.
Muswada huo ulipelekwa na Gavana Greg Abbott ambae ameahidi
kuutia saini ili iwe sheria ambapo itakua ruhusa kwa Mtu yeyote mwenye miaka 21
na kuendelea kubeba Bunduki japo waliowahi kuwa na rekodi za uhalifu
hawatoruhusiwa

Post a Comment