QUEEN SENDIGA MPINZANI WA KWANZA SERIKALINI

SIKU chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kutoa kauli kuwa atafanya kazi na mtu yeyote bila kujali itikadi yake ya kisiasa, leo ameiishi baada ya kumteua Mgombea Urais wa Chama Cha Upinzani cha Alliance For Democratic Change (ADC), katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020, Queen Sendiga kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
Queen Sendiga
anachukua nafasi ya Mkuu wa Mkoa huo, Ali Hapi ambaye amehamishiwa mkoa wa
Tabora.
Wakati wa utawala
wa serikali ya awamu ya tano chini ya hayati John Pombe Joseph Magufuli,
viongozi wawili waliingizwa katika utumishi serikalini wakiwa bado viongozi wa
vyama vya upinzani.
Hao ni aliyekuwa
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira ambaye wakati huo alikuwa Mwenyekiti
wa Taifa wa Chama cha ACT na aliyekuwa kiongozi mwingine wa chama hicho, Dk.
Kitila Mkumbo ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji.
Wakati wa kampeni
zake za kuutafuta urais wa Tanzania, Queen alikuwa akipiga kampeni zake kwa
kuwafuata akina mama kwenye shughuli zao, akienda sokoni, stendi za mabasi na
hata katika mihangaiko mingine ya wanawake.
Aidha, wakati wa
kampeni hizo, alikuwa akimuunga mkono aliyekuwa mgombea urais wa CCM, Hayati
John Magufuli na mara kadhaa, alisikika akimuomba Rais Magufuli amkumbuke
katika utawala wake.

Post a Comment