PROFESA JAY AFUNGUKA KUHUSU DIAMOND

PROFESA Jay ameungana na wasanii Irene Paul na Kajala Masanja kupiga kampeni za kutaka taifa limpigie kura Diamond katika tuzo za BET International Awards.
"Naomba LEO niandike kidogo,
Mwaka 2006 nilichaguliwa kuwania TUZO za MTV BASE ambazo zilifanyika katika
jiji la ABUJA - NIGERIA, Nilikuwa nimechaguliwa kugombea Category Ngumu sana ya
BEST HIP HOP ARTIST ambapo nilikuwa nagombea na JAY Z, LIL WAYNE na msanii wa
NIGERIA anaitwa 9ICE, Nilikuwa Msanii pekee kutoka TANZANIA na nilikuwa
nimeambatana na @josephkusaga @kelvin.twissa kutokana na Nafasi zao kwenye MUZIKI wa AFRIKA,
Kwa kweli nilijua kabisa kuwa SITASHINDA kwenye nafasi hiyo
kutokana na ubora wa wale watu nguli niliokuwa nashindana nao ila niliona hiyo
ni nafasi yangu kubwa na ya kipekee ya kuitangaza nchi yangu na utamaduni wetu
na nilivaa vazi ililowavutia wengi VAZI la KIMASAI na nilipewa Heshima kubwa ya
kukabidhi TUZO kwa mmoja wa washindi. Kilichotushangaza sisi tuliotoka TANZANIA
ni CAMPAIGN ya nchi nzima ya WANAIJERIA ya kuhakikisha msanii wao 9ICE
anashinda TUZO hiyo na sio TUZO hiyo pekee bali TUZO zote ambazo Wanaijeria
wanagombea, Ilikuwa ni KAMPENI kubwa ya nchi nzima , KAMPENI hiyo iliongozwa na
WAZIRI wao wa SANAA na UTAMADUNI sambamba na WAZIRI wao wa UTALII, Nia yao
ilikuwa kuwauza wasanii wao wa nchi yao kwa TAIFA lao, Mwisho kwenye Category
yetu msanii 9ice alishinda mbele ya JAYZ, LILI WAYNE na Mimi, Binafsi sikuwahi
kumsikia kabisa mpaka leo ni miaka 15 imepita sijui hata alishawahi kuimba kitu
gani, Kwa mwaka huo zaidi ya asilimia 90 za AWARDS zilibakia Kwa WANAIJERIA,
Hii ina ni funzo kubwa sana kwetu Watanzania kuwa anaposimama
MTANZANIA yeyote kugombea TUZO yeyote au jambo lolote Duniani ni lazima
tusimame nae pamoja bila kujali Makundi yetu , Itikadi zetu, dini zetu wala
makabila yetu maana hapo Inasimama TANZANIA na sio mtu mmoja mmoja,
Kwa MFANO huu wa NIGERIA Nitumie nafasi hii ya muhimu
kuwaomba WATANZANIA wote kwa umoja wetu tusimame pamoja na tumsapoti Kijana
wetu @diamondplatnumz ambae ni msanii pekee wa TANZANIA na anasimama kidete
kuiwakilisha TANZANIA kwenye TUZO kubwa za BET aweze kushinda AWARD hii kwa
manufaa ya TAIFA letu, mlango wa DIAMOND ukifunguka, Mlango wa wasanii wa
TANZANIA umefunguka , LETS GO GET DEM 💥💥💥💥 Mungu ibariki TANZANIA, Mungu mbariki @diamondplatnumz 🙏

Post a Comment