BOSI TAKUKURU ATHIBITISHA SABAYA KUKAMATWA


Mwananchi - Rais Samia Suluhu amemteua Kamishna Msaidizi... | Facebook

 MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), Kamishna wa Polisi Salum Hamduni AMETHIBITISHA kuwa wanamshikilia aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya kwa maojiano tangu May 25 mwaka huu.

Kamishna Hamduni amesema Sabaya hakukamatiwa Arusha kama vyombo mbalimbali vya habari vilivyoripoti, bali alikamatwa jijini Dar akiwa na watu wawili waliotambuliwa kuwa ni "mabaunsa" wake na wote wapo mahabusu kwa mahojiano.

Amesema wanaendelea kuhojiwa na wakipatikana na kesi ya kujibu watafikishwa mahakamani.!

No comments