PICHA YA MAKONDA YANOGESHA MITANDAO


eka.jpg

 PICHA ya aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni kabla ya kupandishwa na kuwa RC wa Dar es Salaam, Paul Makonda, imegeuka kuwa kivutio baada ya kuzua mijadala mingi katika mitandao ya kijamii.

Picha hiyo inayomuonyesha kiongozi huyo wa zamani akiwa amepumzika huku akipata bites na juisi, inamuonyesha akiwa amenenepa, tofauti na wajihi wake wakati akiwa ofisini kabla hajaondolewa mwaka 2020.

Watu wamekuwa na mtazamo tofauti juu ya kiongozi huyo ambaye licha ya kukaa ofisini kwa muda mchache, lakini jina lake lilikuwa kubwa mno, hasa katika kipindi cha uongozi wa Rais wa awamu ya tano, John Pombe Magufuli.

No comments