MTAKA AWALIPUA VIONGOZI WAJINGA WANAOBEZA SEKTA BINAFSI

WAKATI viongozi wengi wa serikali walioteuliwa au kuchaguliwa na wananchi wamekuwa kama vile hawaoni mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya nchi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amewalipua viongozi wa namna hiyo na kuwaita WAJINGA.
Akizungumza wakati wa kikao cha kuwekeana
mkakati mkoani Dodoma, RC Mtaka amesisitiza uongozi unapatikana kwa kuchaguliwa
kwa kura au kuteuliwa, Lakini kuna wakati wananchi wanaweza kumpigia kura mtu
mjinga na akawa kiongozi wao na kujiona Serikali ni kila kitu lakini sio sekta
binafsi.
Hata hivyo anasema yawezekana mtu akateuliwa pia akawa mjinga na kuanza
kudharau sekta binafsi, Anasema kwake sekta binafsi ni ufunguo wa maendeleo, hivyo
amewaomba watumishi kuheshimu sekta binafsi.
Mkuu wa mkoa wa Dodoma RC Mtaka anasema viongozi wa Serikali waheshimu sekta
binafsi kwani kufanya kazi binafsi kunahitajika akili kubwa, Viongozi wengi wa
Serikali hawawezi hata kujiajiri ingawa wanalipwa mshahara wengine mpaka milioni
mbili, mpaka wakistaafu ndio wanaheshimu sekta binafsi.

Post a Comment