OMBAOMBA WA WHEEL CHAIR WATOWEKA DAR

WAKATI agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makala la kutaka watu wote wanaojihusisha na ombaomba kuondolewa, imebainika kuwa wale ombaomba waliokuwa wakitembezwa kwenye viti maalum vya wasiojiweza (Wheel chair) hawapo tena mitaani.
Habari ambazo bado
Ojuku blog haijazithibitisha zinadai, wananchi hao walikuwa ni mradi wa mtu,
aliyewakusanya kutoka mikoani na kuwajaza katika nyumba yake, akiwapatia
mahitaji muhimu, kisha akiajiri watu wa kuwatembeza ambao walikuwa wakimletea
hesabu.
Vyanzo vinasema mtu
huyo amekamatwa na uchunguzi unaendelea.

Post a Comment