MCHEZAJI WA TIMU YA TAIFA UFARANSA AKUBALI UBALOZI WA HIYARI UTALII TANZANIA


Mamadou Sakho - Le Gladiateur [HD] | Soccer world, Paris saint-germain,  Soccer

MWANASOKA wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Mamadou Mamadou Sakho, amekubali ombi la kutakiwa kuwa balozi wa hiyari wa utalii wa Tanzania kufuatia ombi lililopelekwa kwake na Bodi ya Utalii nchini, TTB.

Sakho ambaye pia ni mchezaji wa Crystal Palace inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza (EPL), alikuwepo nchini hivi karibuni na familia yake, akipumzika katika mbuga kadhaa, ikiwemo Serengeti.

Sakho alikubali ombi hilo wakati alipokutana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TTB, Betrita Lyimo katika Hifadhi ya Bonde la Ngorongoro.


No comments