EMANUEL OKWI NAHODHA THE CRANES


Ugandan striker Emmanuel Okwi warns Tanzania's Taifa Stars ahead of Afcon  showdown | Goal.com

EMANUEL Okwi, kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Uganda anayecheza soka la kulipwa nchini Misri katika klabu ya Al Ittihad Alexandria amechaguliwa kuwa nahodha wa timu yake ya taifa akirithi mikoba ya mlinda mlango maarufu David Onyango aliyestaafu rasmi kuichezea timu hiyo.

Okwi mwenye umri wa miaka 28, alipata kuwika na majogoo ya soka Tanzania Simba SC akiwa sehemu ya kikosi cha dhahabu cha klabu hiyo 2010-13 alipocheza mechi 38, akitupia kambani goli 18 na kutengeneza magoli 27.

Okwi alirudi tena Simba SC msimu wa 2014-15 akitokea Young Africans , ambapo alicheza mechi 18 na kufunga magoli 9 huku akitengeneza 7.

Akiwa na Simba SC msimu wa 2014-15, Okwi alicheza mechi 20 tu na kutupia kambani goli 16!.

Emanuel Okwi anatajwa ni mmoja wa viungo wakubwa wa nje aliyepata mafanikio makubwa akiwa Tanzania, aliweza dhihirisha ubora wake tena kipindi cha 2017-19 akiwa na Simba SC alipocheza mechi 50 na kufunga magoli 36 akitengeneza magoli 16.

Ndani ya klabu yake ya sasa, ameweza kucheza mechi 14 tu akifunga magoli mawili (2) huku akifanikiwa kutengeneza magoli 7.

Alianza kuichezea timu yake ya taifa mwaka 2011 na kufanikiwa kucheza mechi 89 na kufunga magoli 26 akitengeneza magoli 4 tu. 

No comments