LAMINE MORO ATIMULIWA KIKOSINI YANGA

NAHODHA wa mabingwa
wa kihistoria nchini, Yanga, Lamine Moro ametimuliwa kambini baada ya kutokea
kwa sintofahamu baina yake na Kocha Nasraddine Mohammed Nabi.
Yanga ambayo ipo Ruangwa
mkoani Lindi kujiandaa kwa mechi ya baadaye jioni ya leo dhidi ya wenyeji
Namungo, imemuamuru beki huyo kisiki raia wa Ghana, kurejea jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa klabu
hiyo, Hassan Bumbuli amenukuliwa akisema Lamine ameamriwa kurejea Dar na kocha
baada ya kutokea sintofahamu baina yao jambo ambalo halikuwa na afya kikosini.

Post a Comment