KIDUKU AKATAZA SKIN JEANS KOREA KASKAZINI





Coronavirus crisis heightens political risks for North Korea's Kim Jong Un  | Arab News

WAKATI vijana kote duniani wakifurahia zama zao kwa kuvaa suruali za kubana maarufu kama Skin Jeans na wakati huo huo wakizilegeza kamalioni, hali ni tofauti nchini Korea Kaskazini.

Rais kijana wa taifa hilo, Kim jong-un ambaye ni maarufu hapa nyumbani kama Kiduku kutokana na aina yake ya unyoaji nywele, amepiga marufuku kali jinzi na suruali zinazobana, akihofia raia wa nchi hiyo kuiga utamaduni wa kimagharibi. 

Kwa Korea Kaskazini kufuata falsafa ya Kikomunisti, imejitengenezea maadui wengi duniani, hasa Ulaya na Marekani ambao wanapinga mfumo wao wa utawala.

Kwa mujibu wa shirika la habari la "Yohap News" kutokea Korea Kusini limelinukuu jarida la Korea Kaskazini katika moja ya machapisho yake limesisitiza kuzuia mila za kimagharibi kuingia nchini humo au wananchi wawe tayari kuona mila na tamaduni zao kupotea hivi hivi. 

Kwa maana hiyo, chunga sana ikitokea unaelekea mitaa hiyo ya dunia.

No comments