HOYCE TEMU ANASTAHILI UBALOZI


NURU THE LIGHT: HOYCE TEMU!!!

KUFUATIA uteuzi uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan jana wa mabalozi na kutajwa kwa jina la Hoyce Temu, wengi wamejawa na mashaka na kujiuliza ni kwa jinsi gani mrembo huyo aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 1999 anaiweza nafasi hiyo.

Ukweli ni kwamba Hoyce, ambaye alijipambanua kama Miss Tanzania pekee kujikita katika shughuli za kijamii hata baada ya kuvua taji hilo, anastahili nafasi hiyo kwani licha ya sifa nyinginezo, alisoma Stashahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Mahusiano ya Kigeni yaani Post Graduate Diploma in Management of Foreign Relations (PGD-MFR) kutoka Chuo cha Diplomasia Kurasini Dar es Salaam na Mozambique-Tanzania Centre for Foreign Relations (CFR). 

Hoyce Temu aliwahi kuhudumu Umoja wa Mataifa Tanzania (UN-Tanzania) kama Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano lakini pia alipata kuhudumu kama Mtaalamu wa Mawasiliano UN-Tanzania (UN Communication Specialist) na pia Mchambuzi wa Mawasiliano au UN Communication Specialist. 

Hivyo Hoyce Temu ana taaluma ya Uhusiano wa Kimataifa na Diplomasia kutoka Chuo cha Diplomasia na zaidi ya hilo ana weledi wa masauala ya kidiplomasia kutokana na kufanya kazi UN ofisi ya Tanzania. 

kwa kifupi, alichosoma Hoyce Temu ndicho walichosoma maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ambao kikanuni ni lazima wasome kozi za Chuo cha Diplomasia (CFR) kama kigezo kimojawapo cha kutoka ngazi moja ya daraja kwenda lingine ili waweze kumudu majukumu yao ipasavyo.

Credit: Jamii Forum

 

No comments