DUH, BILL COSBY 'KUOZEA JELA'

HAPO ndipo ilipo tofauti ya nchi zetu za Afrika na wenzetu barani Ulaya na Marekani. Hakuna aliye juu ya sheria, bila kujali mkwanja unaomiliki, umaarufu au ushawishi wa namna yoyote kwa jamii.
Mchekeshaji huyo mkongwe na mahiri duniani Bill Cosby, akitamba na kipindi chake cha The Cosby Show, mwenye umri wa miaka 83, alihukumiwa jela kwa muda wa miaka mitatu hadi kumi baada ya kupatikana na hatia ya kuwawekea madawa ya kulevya wanawake na kisha kuwalawiti mwaka 2004.
Cosby alikuwa ametaka apewe ruhusa ya kutumikia
kifungo chake akiwa nyumbani, lakini CNN inaripoti kuwa Bodi ya Parole ya
Pennsylvania imetoa uamuzi wake mnamo Mei 11, kuwa Cosby lazima akamilishe
program ya elimu na ushauri anaotakiwa kupewa kabla ya kuruhusiwa kuingia
kwenye orodha ya watu wanaopendekezwa kutumikia kifungo chao nyumbani.
Msimamo wa Bill Cosby toka mashtaka haya kufunguliwa
haujabadilika, akisema Hana hatia, hawezi omba radhi kwa makosa ambayo
hajafanya na hana mpango wa kuhudhuria program hizo za matibabu. Nyota huyu wa
"The Cosby Show" hapo awali alisema anatarajia kutumikia kifungo
chake kamili cha miaka 10 jela.

Post a Comment