BIFU LA WANANDOA WALIOPENDWA LAENDELEA

 

Angelina Jolie hints how divorce from Brad Pitt made her return to acting |  English Movie News - Times of India

KATIKA ulimwengu wa filamu na mastaa wake, hakuna ndoa iliyowahi kupendwa na kutakiwa idumu zaidi ya ile ya mastaa wawili Hollywood, Brad Pitt na mkewe Angelina Jolie. 

Lakini wawili hao, wakiwa na watoto wao sita, waliishi maisha ya ndoa kwa miaka miwili tu kabla ya kutenganishwa na mahakama. Kesi yao kubwa ni namna ya kuishi na watoto wao, kila mmoja akidai haki hiyo.

Jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo juu ya haki ya kulea watoto, iliyochukua muda wa miaka miwili ametoa hukumu yake kuwa Brad na Angelina watashirikiana kulea watoto wao pamoja.


Ingawa kesi imeisha ila bado vita inaendelea, Angelina amepanga kukata rufaa sababu hataki watoto hao waishi na baba yao akitoa sababu za mazingira hatarishi anayoishi Brad Pitt.

Brad Pitt na Angelina Jolie waliishi kwenye ndoa kwa miaka miwili tu na kutengana mwaka 2016, Walitenganishwa kisheria mnamo Aprili 2019 na wamekuwa wakigombania watoto wao tangu wakati huo.

No comments