BAADA YA JINA LAKE KUKOSEWA TFF, DILUNGA: NGUVU ZOTE SIMBA

SIKU chache baada ya kutokea sintofahamu kuhusu kukosewa kwa jina lake ndani ya kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, kiungo wa Simba Hassan Dilunga amesema kwa sasa nguvu zake zote amezielekeza kuisaidia klabu yake kutetea taji lake la nne la Ligi Kuu na pia Kombe la Shirikisho.
Jina la Hassan Dilunga liliwekwa kwenye orodha ya majina ya kikosi cha wachezaji 27 wa Taifa Stars juzi kisha baadaye Shirikisho la Soka la Tanzania, (TFF) likaeleza kuwa walikosea kimaandishi, wakisema aliyekusudiwa ni Mudhathir Yahya.
"Nimewekeza juhudi zangu zote
kufanya vizuri na kuiwezesha klabu yangu ya Simba kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu
kwa mara ya nne mfululizo pamoja na Kombe la Shirikisho."

Post a Comment