AKINA MDEE WANAWEZA SAMEHEWA CHADEMA


Chadema chairman Freeman Mbowe to be a free man today - The Citizen

HUKU wanachama na mashabiki wa chama kikuu cha upinzani nchini, Chadema wakitaka wanachama 19 waliovuliwa uanachama kwa kosa la kujitangaza ubunge wa viti maalum na kuapishwa wafukuzwe, kuna dalili kuwa wabunge hao wanaweza kusamehewa.

Dalili hizo zinakuja kufuatia kauli ya Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Freeman Mbowe aliyoitoa jana akiwa katika kikao cha ndani mjini Bunda mkoani Mara.

Mbowe alikaririwa akisema endapo wanachama hao 19 waliofukuzwa wakirudi na Baraza Kuu likawasamehe hakuna shida yoyote, anawafahamu vizuri kwani wamekuwa watu wake wa karibu zaidi ya wanachama wanavyofahamu.

No comments