CARLINHOS ABWAGA MANYANGA YANGA


Carinhos safi Yanga, afanya mambo African Lyon | maliyaga

HABARI ambazo hazijathibitishwa za hivi karibuni zinadai kiungo mshambuliaji wa Yanga, Carlos Sténio Fernandes Guimarães do Carmo maarufu kama Carlinhos, amevunja mkataba na klabu ya Yanga na amerejea kwao.

Sababu za kuvunja mkataba huo hazijawekwa wazi, lakini mojawapo ya sababu za kiungo huyo raia wa Angola, ni za kifamilia.

Msemaji wa mabingwa hao wa kihistoria, Hassan Bumbuli alipoulizwa kuhusu suala hilo, hakuwa wazi, akidai hata yeye ameliona mitandaoni tu, lakini hana mawasiliano na viongozi ili kujua kinachoendelea.

No comments