WAZIRI CHAMURIHO ATOA MAAGIZO KIWANJA CHA NDEGE IRINGA
Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Mkoa wa Iringa,
Kindole Daniel akielezea jambo kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi, Dkt.
Leonard Chamuriho (Wa Tatu kushoto mbele) wakati Waziri huyo alipotembelea mradi
wa Ukarabati wa Kiwanja cha ndege cha Iringa kujionea maendeleo yake.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhandisi, Dkt.
Leonard Chamuriho, ameitaka Kampuni ya kikandarasi ya Sino Hydro Corporation
kutoka China kuhakikisha kuwa wanakamilisha kazi ya ukarabati wa Kiwanja cha
ndege cha Iringa kwa muda uliopangwa ili kuruhusu ndege kubwa kuweza kutua katika
kiwanja hicho.
“Kama mnavyoona, sasa hivi huduma ya ndege ya ATC
imesimama kwa sababu ya ukarabati huu, hakikisha Mkandarasi unatekeleza kazi hii
kwa haraka kama mkataba unavyosema, wananchi wa hapa wanasubiria kwa hamu Kiwanja
hiki”, amesema Chamuriho.
Aidha, amemtaka Meneja wa Wakala wa Barabara
(TANROADS), Mkoa wa Iringa, Mhandisi, Kindole Daniel, kukaa na Mkandarasi huyo kuona
namna ya kuunganisha awamu mbili za ukarabati kama zilivyoainishwa na Mkandarasi
ili kukamilisha mapema kazi hiyo.
Amesisitiza kwa Meneja huyo kuhakikisha kuwa, wananchi
wa maeneo jirani ya mradi huo wanapata ajira ili waweze kunufaika na mradi huo,
pia kuweka matangazo kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuhusu ajira za kitaalamu ambazo
zinatolewa na Mkandarasi huyo ili wataalamu wazawa nao kuweza kuomba nafasi hizo.
Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara
(TANROADS), Mkoa wa Iringa, Mhandisi, Kindole Daniel, amesema kuwa mradi wa ukarabati
wa Kiwanja cha ndege cha Iringa unahusisha matengenezo makubwa ya njia ya kuruka
na kutua ndege ya sasa yenye kiwango cha lami nyepesi, ujenzi wa eneo la
usalama, njia ya michepuo ya ndege, maegesho mapya ya ndege, jengo la muda la
abiria na mnara wa muda wa kuongozea ndege.
Ameongeza kuwa, mradi huu pia unahusisha ujenzi wa jengo
la zimamoto, ujenzi wa jengo la kituo cha nishati na kuweka taa za ardhin ikwenye
njia ya kuruka na kutua ndege.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Iringa ameomba ujenzi huo ufanyike
kwa awamu moja ili uishe haraka kwani wananchi wa Mkoa huo wanapata tabu kwa sasa
kutokana na Kiwanja hicho kupokea ndege ndogo pekee.
Mrad iwa Ukarabati wa Kiwanja cha ndege cha Iringa,
ulisainiwa mwezi Mei mwaka jana ,ambapo Ukarabati wake unahusisha kazi mbalimbali
ikiwemo ujenzi wa njia ya kuruka na kutua ndege kutoka urefu wa kilometa 1.6
hadi kufikia kilometa 2.1 na hivyo kupelekea hata ndege za masafa ya kati kuweza
kutua kwa urahisi pindi ukarabati huo utakapokamilika.
Imetolewa
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi

Post a Comment