Zlatan: Sijamuona Ronaldo Italia, Ronaldo ni mmoja tu, yule Mbrazil
Pichani kulia, Zlatan akisalimiana na Ronaldo Mreno wakiwa na timu zao za Taifa na kushoto, Msweden huyo akimkabidhi jezi legendari wa Brazil, Ronaldo de Lima
Mtandao wa AiScore
Sports, unaojihusisha na habari za michezo na wanamichezo, umeripoti leo kuwa
mshambuliaji wa Sweden na AC Milan, Zlatan Ibrahimovic amemponda nyota wa
Juventus, Christiano Ronaldo, raia wa Ureno.
"Unaniuliza
kama nimemuona Ronaldo halisi Italia? Sijamuona, kuna Ronaldo mmoja tu, yule Mbrazil."
"Cristiano
Ronaldo alijisajili timu ambayo imeshinda taji la Serie A mara saba mfululizo.
Kwenda katika klabu kama hiyo hupati changamoto. Kama ninataka changamoto
kweli, ningeenda Juventus ikiwa Serie B nipambane kuipandisha na kuiweka
juu."

Post a Comment