Adriano auza nyumba, ahamia hotelini


 Adriano Leite Ribeiro, maarufu kama Adriano, nyota wa zamani wa Brazil, haishi vituko. This time, mshambuliaji huyo wa zamani wa Parma na Inter Milan za Italia, ameuza nyumba yake yenye thamani ya paundi milioni 1.2 sawa na shilingi za kitanzania 348000000 (3.48bilioni).

Nyumba hiyo ipo eneo liitwalo Barra da Tijuca, linalokaliwa na watu wa daraja la juu magharibi ya jiji la Rio de Janeiro nchini Brazil.

Lakini baada ya kuiuza nyumba hiyo hiyo, aliacha kila kitu kilichomo ndani yake, isipokuwa medali zake tu alizotwaa enzi akicheza soka na kwenda kupanga chumba hotelini ambako analipa dola 10 (sawa na shilingi za kitanzania 23,000) kwa siku.

Adriano, ambaye wakati akiibuka katika soka miaka ya mwanzoni mwa 2000, akitajwa kama mrithi wa Ronaldo de Lima, alishindwa kufikia matarajio baada ya kuanza maisha ya starehe na unywaji pombe uliopitiliza.

 

No comments