WATU WAKANYAGANA KUMUAGA MAGUFULI
Ni full. Uwanja wa
Uhuru jijini Dar es Salaam wenye uwezo wa kuingiza watu 40,000 waliokaa, leo
umejikuta ukizidiwa, baada ya watu wengi kuliko maelezo kuingia katika harakati
za kumuaga Mwamba, Dokta John Pombe Joseph Magufuli.
JPM aliyefariki
Machi 17 mwaka huu, anaagwa kwa mara ya mwisho na wakazi wa Dar es Salaam leo
kabla ya jioni kupelekwa Dodoma ambako wakazi wake watapata fursa hiyo kesho,
itakayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri.
Ratiba pia
inaonyesha wananchi za Zanzibar na Mwanza nao watapata fursa ya kuaga kabla ya
mwili wake kulazwa katika nyumba yake ya milele, kijijini kwao Chato Mkoani
Geita Ijumaa hii.

Post a Comment