Simba waonyesha maana ya timu bora
Sare ya bao 1-1 iliyopata Simba jana dhidi ya Prisons ya Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, umethibitisha pasi na shaka kuwa mabingwa hao wa nchi mara tatu mfululizo ni timu bora uwanjani.
Jambo moja tu ndilo unaloweza kusema, timu hiyo ilikosa bahati. Kwa nini? Ilitawala mchezo tokea dakika ya kwanza hadi ya tisini. Ilikosa penati ya mapema kabisa, ikakosa nafasi nyingi mchezoni hasa wapinzani wao wallipobaki 10 uwanjani kwa makosa yha kishamba ya beki wao.
Lakini hawakukata tamaa, waliendelea kushambulia kwa soka safi, spidi na nidhamu ya hali ya juu hadi walipofanikiwa kusawazisha sekunde ya mwisho.
Prisons walijitahidi sana, lakini kama ambavyo timu zote ndogo zilivyo, hujitoa sana zinapokutana na timu kubw, hasa Simba na Yanga. Sare waliyoipata imewaongezea pointi moja muhimu, japo haiwapi uhakika wa kubaki Ligi Kuu kama wasipoendelea kupambana

Post a Comment