Kufungwa WhatsApp kwawavuruga watu
KUSUDIO la serikali kuthibiti matumizi ya
mtandao wa WhatsApp limepokelewa kwa hisia tofauti, huku wananchi wengi
wakivurugwa, kwani hawaelewi nini hasa lengo la jambo hilo.
Siku chache zilizopita, Waziri wa Habari na
Teknolojia, Faustine Ndungulile alisema matumizi ya mtandao huo katika video
calls, simu za kawaida na sms, yamekuwa yakichangia kwa kiwango kikubwa
kuporomoka kwa mapato kwa makampuni ya simu na mapato ya serikali.
Hivyo, wanataraji kudhibiti matumizi hayo ili
kuwafanya watumiaji hao kuchangia gharama hizo, jambo linalopigwa na wadau
wakidai juhudi hizo ni kupingana na ukuaji wa teknolojia, jambo ambalo
halitafanikiwa.
"Serikali haiwezi kushindana na ukuaji wa
teknolojia, badala ya kutafuta njia za kupambana nayo, ni vyema iangalie namna
ya kukabiliana nayo kwa ubunifu wa namna nyingine ya wao kuweza kupata
mapato," anasema mwanafunzi mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
aliyejitambulisha kwa jina moja na Vivian.
"Teknolojia inakuja kwa ajili ya
kurahisisha maisha, sasa wewe unakataa unataka watu bado waendelee kuishi
kizamani, kweli?" alihoji mwananchi mwingine aliyefikiwa na
Batablogspot.com.
"Mimi nimekuwa nikifanya biashara na kupata
wateja wangu kutoka mbali na nilipo kwa kuongeo na kuwaonyesha bidhaa zangu
kupitia video call, hii imenirahisishia maisha. Sasa serikali gani ya wanyonge
inataka watu waendelee kutaabika wakati teknolojia inawasaidia?
"Cha msingi wao wakae na kubuni namna ya
kukabiliana na changamoto hii. Makampuni ya simu yapunguze gharama za vifurushi
wateja wataongezeka na serikali itapata mapato. Yaani serikali inataka
kuyasaidia makampuni ya simu kwa gharama za wanyonge?"

Post a Comment