DC akemea wafuga fisi mijini
Mkuu wa Wilaya ya Nyang'wale Wilson Shimo ameanzisha operesheni maalum ya nyumba kwa nyumba ili kuwadhibiti Fisi ambao wamekuwa wakiwaua na kuwajeruhi watoto. Fisi hao ambao inadaiwa hutumiwa na wenyeji kwa shughuli za usafiri walisababisha mauaji ya watoto watatu huku watano wakijeruhiwa vibaya.
Akizungumzia matukio ya vifo hivyo mkuu huyo wa wilaya anasema tayari fisi 28 wameuawa katika operesheni hiyo na msako unaendelea usiku na mchana.Kaimu afisa mifugo na uvuvi wilaya ya Nyangwale,. Dickson Msumari anasema fisi hao ni tishio na wamekuwa wakiingia mpaka maeneo ya mjini nyakati za mchana na kuua watoto.
Aidha, Mbunge wa jimbo la nyangwale Hussein Nassoro anasema wameomba nguvu kutoka mkoa Shinyanga ili kuwawinda hao.
Chanzo: ITV

Post a Comment