Samia kuapishwa leo, JPM kuzikwa Chato


 Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ataapishwa leo asubuhi hii saa nne, Ikulu jijini Dar es Salaam kuwa Rais wa Sita wa Tanzania.

Mama Samia anachukua nafasi ya Rais John Magufuli, aliyetangazwa kufariki Jumatano Usiku Machi 17, 2021.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Hassan Abbas, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mwili wa JPM utaagwa katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Mwanza, kabla ya kufikishwa Chato kwa mazishi.

 

No comments