SAFARI YA MWISHO KABISA YA MAGUFULI
RAIS wa awamu ya
Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, leo atafanya
safari ya mwisho kabisa duniani, wakati mwili wake utakapowasili kijiji
alichozaliwa cha Chato, mkoani Geita.
Safari hiyo
ilianzia katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambako msafara wa magari
uliondoka, baada ya kuagwa na umati wa maelfu kwa maelfu ya wananchi
waliojitokeza kutoa heshima zao za mwisho.
Magufuli,
aliyepachikwa majina mengi ya utani kama vile Jiwe, Mwamba na Jeshi,
alitangazwa kufariki Machi 17 mwaka huu, kwa maradhi ya moyo.
Kabla ya safari
yake ya mwisho hapo jana, aliagwa kwa siku mbili mfululizo jijini Dar es
Salaam, siku moja Makao Makuu ya Nchi, Dodoma, siku moja pia katika sehemu ya
pili ya Muungano, huko Zanzibar.
Magufuli anakuwa
rais wa kwanza wa Tanzania kufariki akiwa madarakani, rekodi ambayo imeandika
rekodi nyingine ya kupata mwanamke wa kwanza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye aliapishwa kuchukua nafasi hiyo kwa
matakwa ya katiba.

Post a Comment