Rais John Joseph Pombe Magufuli afariki
BAADA ya wiki takribani mbili za sintofahamu ya wapi alipo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na hali yake kiafya, hatimaye leo Machi 17, 2021 saa tano usiku, Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, ametangaza kifo cha kiongozi huyo mzalendo.
Mama Samia ameliambia Taifa kuwa Rais Magufuli alifariki leo saa 12 asubuhi katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli amefariki kwa maradhi ya moyo , alilazwa March 6 2021 katika Hospitali ya Jakaya Kikwete na kuruhusiwa March 7 na kuendelea na majukumu yake”
“March 14 alijisikia vibaya na akarudi Hospitali ya Mzena ambapo aliendelea na matibabu hadi umauti unamkuta, Nchi yetu itakuwa na maombolezo ya siku 14 na bendera zitapepea nusu mlingoti”amesema Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu
Post a Comment