Huyu ndiye John Joseph Pombe Magufuli


 

 

 

·         1959- Azaliwa Chato kaskazini magharibi mwa Tanzania

·         1995- Achaguliwa kuwa mbunge kwa mara ya kwanza

·         2000- Ateuliwa kuwa Waziri

·         2015- Achaguliwa kuwa rais kwa muhula wake wa kwanza

·         2020- Achaguliwa kwa kipindi cha pili kuwa rais

·         2020 Novemba tarehe 5 – Aapishwa kwa muhula wa Pili

·         2021 Machi Tarehe 7- Uvumi unaanza kuenea kuhusu aliko rais Magufuli baada ya kukosa kuonekana kwa muda wa wiki moja

·         2021 Machi tarehe 11 – Vyama mbali mbali vya Upinzani nchini Tanzania vyataka kujua hali ya rais Magufuli na aliko

·         2021 Machi Tarehe 12 -Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akana kwamba rais Magufuli anaugua asema yupo ‘ buheri wa afya na anaendelea kuchapa kazi’

·         2021 Machi Tarehe 15 – Makamu wa Rais Samia Suluhu awapa Watanzania ‘salamu’ kutoka kwa Rais Magufuli huku hofu ikizidi kuhusu hali yake na aliko

·         2021 Machi, tarehe 6 – Alazwa katika taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete kwa tatizo la moyo la mfumo wa umeme

·         2021 Machi tarehe 7 – Aliruhusiwa kurejea kazini

·         2021 Machi tarehe 14 – Alikimbizwa Hospitali ya Mzena Dar es Salaam kuendelea na matibabu

·         2021 Machi tarehe 17 saa kumi na mbili jioni – Magufuli afariki dunia

·         2021 Machi tarehe 17 Usiku – Makamu wa rais Samia Suluhu atangaza kupitia runinga kifo cha rais Magufuli .Siku 14 za maombolezo zatangazwa.Bendera kupeperushwa nusu mlingoti.

 

 

No comments