Raila atoka Hospitalini

 


KIONGOZI wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga ameruhusiwa kutoka hospitalini alikokuwa amelazwa baada ya kupatwa na virusi vya korona, Covid 19.

Raila, Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya mwenye umri wa miaka 76, alilazwa tangu Machi 9 mwaka huu, baada ya daktari wake kusema alikuwa akijisikia maumivu ya mwili na uchovu.

Ikiwa ni mwaka mmoja toka Kenya ipate mgonjwa wa kwanza, nchi hiyo imerekodi watu 110,000 kuugua ugonjwa huo, 87,903 wakiripotiwa kupona na vifo zaidi ya watu 2,000.

Mwanzoni mwa ugonjwa huo, Utawala wa Rais Uhuru Kenyatta ulipiga marufuku mikusanyiko ya kisiasa, kufunga sehemu kubwa ya shughuli za kijamii na kiuchumi.

 

No comments