Diamond ampaisha Haji Manara
Diamond Platnum, msanii maarufu zaidi wa
Tanzania, ambaye pia ni CEO wa Wasafi Media, jana usiku alimtembelea Msemaji wa
Simba Haji Manara, nyumbani kwake, Mikocheni jijini Dar es Salaam.
Diamond aliyeongozana na msanii aliye chini ya
lebo yake ya WCB, Mbosso pamoja na baadhi ya staff wake wa Wasafi, alishiriki
pia chakula cha usiku, kilichoandaliwa na mke wa Manara, Naheeda
Abdallah.
Hii inakuja siku chache baada ya msemaji huyo kuwa katika
mzozo mkubwa uliomalizwa kiutu uzima na mtangazaji wa Wasafi FM, Maulid Kitenge.
Diamond ambaye jina lake lingine la utani ni Simba, ni shabiki
kindakindaki wa klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi

Post a Comment