Mwambusi na viatu vya Kaze kwa muda
KOCHA mkongwe wa soka la Tanzania, Juma Mwambusi, kwa mara nyingine amerejea katika klabu ya Yanga, lakini tofauti na mara zote alizoenda kama mwalimu msaidizi, safari hii anaingia kama Kocha Mkuu wa muda.
Hiyo inafuatia kutimuliwa kwa benchi lote la
ufundi siku chache zilizopita, kufuatia matokea yasiyo ya kuridhisha chini ya
aliyekuwa kocha mrundi, Cedric Kaze na msaidizi wake, Nizar Khalfan.
Mwambusi alipata kufanya kazi na Kaze akiwa kama
msaidizi wake, kabla ya kuacha nafasi hiyo kwa ajili ya matibabu miezi michache
iliyopita.
Uongozi wa klabu ya Yanga umesema upo katika
mchakato wa kutafuta kocha mpya atakayeweza kurejesha heshima ya klabu hiyo
yenye ubingwa wa kihistoria katika soka la Tanzania

Post a Comment