Harmonize usishindane na Daimond
Konde Boy, ameondoka WCB kitambo sasa. Huko alikoenda akaanzisha lebo yake ya Konde Gang. Kama ambavyo yeye alishikwa mkono na Diamond Platnum alipoingizwa Wasafi Classic Baby, naye amemkamata mkono bwana mdogo Ibrah. Yes, Ibra anafanya vizuri na ni nyota njema.
Na hata Harmonize mwenyewe, amejitahidi sana kubakia masikioni na machoni mwa mashabiki wake, kwani tokea ameondoka pale Wasafi, amekuwa akitoa ngoma kadhaa na v ideo zenye viwango. Wapo watu ambao wanaamini kijana huyo kutoka Mtwara, anaweza kuiga nyayo za Simba na kuweza kufanikiwa kuifanya Konde Gang iwe kubwa na imara.
Lakini ukimfuatilia sana Konde Boy, unagundua kwamba pamoja na kuondoka pale kwa Mondi, kuna kitu hakiko sawa. Licha ya yeye mwenyewe kusema hadharani mara kadhaa kwamba anamheshimu sana Diamond na kumuona kama baba yake kimuziki, lakini ukisikiliza baadhi ya mipini yake, unagundua kuna jambo sehemu haliko sawa.
Inaonekana kama kuna sehemu hakutendewa haki, kwani amekuwa akilalamika lalamika hivi. Anaimba nyimbo zenye mafumbo kuonyesha kuwa pale 'nyumbani' hapako sawa. Nini tatizo Harmo?
Ushauri kwa Harmonize ni kuwa Diamond hivi sasa yupo mbali sana kushindana naye, iwe kwa maneno au kwa vitendo. Lakini anawezekana. Njia nzuri ya kupambana na Mondi ni kufanya kazi kwa bidii, kuheshimu ukubwa wake na kuiga mazuri anayofanya yanayomuweka kule juu aliko, si vinginevyo

Post a Comment