Magufuli sasa kuzikwa Machi 26, kuagwa pia Zanzibar
Ratiba ya mazishi ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli imefanyiwa marekebisho madogo ambapo sasa baada ya kuagwa Dodoma, mwili wake utapelekwa Zanzibar ambako utaagwa Machi 23 na kuelekea Mwanza siku itakayofuata.
Mwili huo utaagwa Mwanza Machi 24 na siku ya Machi 25, itakuwa zamu ya wananchi wa Chato na maeneo ya jirani kuaga kabla ya mazishi yake kufanyika siku ya Machi 26, 2021

Post a Comment