Dar kumuaga Magufuli kwa siku mbili


 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge ametoa ratiba na utaratibu wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Dkt. John Magufuli ambapo Mkoa wa Dar es salaam umepewa siku mbili za kutoa heshima za mwisho.

Akitoa ratiba hiyo RC Kunenge amesema kesho Jumamosi March 20 kuanzia saa 1:00 -3:00 asubuhi itafanyika Misa takatifu Kanisa Katoliki Mt. Petro, saa 3:00 - 3:30 asubuhi, mwili wa Marehemu utawasili Uwanja wa Uhuru, saa 3:30 - 4:30 asubuhi itafanyika Misa takatifu ambapo saa 4:30 asubuhi hadi saa 9: 30 alasiri Viongozi wa Serikali, Vyama vya siasa, Wafanyakazi na Taasisi za Umma watatoa heshima za mwisho na saa 9:30 - 12:00 Wananchi watatoa heshima za mwisho.

Kunenge amesema Jumapili saa 2:00 asubuhi mwili wa Marehemu utawasili Uwanja wa Uhuru, saa 2:30 asubuhi hadi saa 10:30 jioni Wananchi watatoa heshima za mwisho ambapo saa 10:30 Jioni hadi saa 11:00 jioni mwili utapelekwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ambapo saa 11:00 jioni hadi Saa 11:45 jioni Mwili utasaririshwa kutoka Dar es salaam kuelekea Dodoma.

 

No comments