MAELFU WAJITOKEZA KUMUAGA JPM


MAELFU ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, leo wamejitokeza kwa wingi kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Tano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli, katika siku yake ya kwanza kuagwa na wananchi.

Katika Uwanja wa Uhuru, maelfu hao walijitokeza licha ya ukweli kwamba leo ilikuwa ni siku rasmi ya viongozi kuuaga mwili huo, kabla ya kesho ambayo ndiyo itakuwa siku rasmi ya kuaga kwa wakazi wa Dar es Salaam na mikoa jirani.

Mwili huo keshokutwa utasafirishwa kuelekea Dodoma ambako utaagwa na kesho yake kuelekea Zanzibar. Rais Magufuli atazikwa kijijini kwake, Chato mkoani Geita Machi 26 mwaka huu.

No comments