DOM HAWANA CHA KUMLIPA JPM

 


WAKAZI wa Jiji la Dodoma hawana cha kumlipa Dokta John Pombe Joseph Magufuli. Amekifanya kile alichokifikiria Mwalimu Nyerere ambacho Ali Hassan Mwinyi, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete walishindwa kukifanya katika miaka 30 ya tawala zao.

Akilihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 2015, mjini Dodoma, Rais John Magufuli alisema ndani ya miaka yake mitano ya kwanza, atahakikisha serikali yote imehamia Dodoma.

Wengi walijua ni majigambo ya wanasiasa. Lakini hadi anakwenda katika kampeni za kuwania urais wa muhula wa pili ambao alishinda, serikali yote ilikuwa imeshahamia Dodoma. Siyo tu hivyo, lakini akaupa hadhi mkoa huo ambao sasa ni Jiji.

Njia pekee ya wao kurejesha shukurani zao kwake, ni kujitokeza kwa wingi, kwa moyo wa dhati, kumpokea na kumuaga. Rest In Peace Magu




No comments