Jiepushe na mambo haya kipindi hiki

Man having a drink in a bar. Closeup side view of a late 40's businessman having a bourbon drink at a local bar after a long day at work.  He's sitting at a bar counter and is totally disconnected, slowly sipping his drink.  Enjoy responsibly! Whiskey Stock Photo


 

Hivi sasa kila mmoja analalamika juu ya hali ngumu ya maisha. Na mambo ni magumu kweli ndugu zangu, ingawa katikati ya msoto huu, wapo ambao wanakula raha hadi wanaboa.

Si mfanyabiashara, si mfanyakazi, si mkulima, si mjasiriamali, kilio ni kilekile, hali mbaya, hamna hela.  Miaka michache iliyopita, ungeweza kukusanya hadi laki tano kwa mwezi kwa 'mizinga' tu, lakini sasa hivi, thubutu, ukipata hata laki shukuru.

Na mizinga hiyo siyo kwamba ulikuwa unawapiga watu wasiwasi, la hasha. Ni watu wako wa karibu ambao wana kazi za kawaida tu huko makazini mwao, wafanyabiashara wa kiwango cha kati tu na hata wajasiriamali.

Lakini sasa hivi kila mmoja anakwambia vyuma vimekaza. Na ushahidi kwamba vyuma vimekaza wala hauhitaji upelelezi wa ofisa wa polisi aliyekubuhu. Unaona tu mwenyewe kwa macho ya kawaida.

Kulikuwa na mabosi wana gari nne hadi tano uani mwao na yote yako barabarani. Moja la mzee, moja la mama, lingine la kusombea vyakula vya mifugo kama ng'ombe, mbuzi na kuku, gari jingine la kuwapeleka na kuwarudisha watoto shuleni na lingine  lipolipo tu attention, lakini liko full tanki.

Sasa hivi unaona, magari matatu yameuzwa, yamebaki mawili, moja la kusombea vyakula vya mifugo la lingine wanatumia wote baba na mama kwenda na kurudi kazini.

Wapo baadhi, hawana hata gari moja. Zamani kila siku kwao ilikuwa sherehe, sasa hivi kukiwa na shughuli majirani wanajiuliza kunani pale?

Huu ni ushahidi kuwa hali ni ngumu kwelikweli na haya yafuatayo ni baadhi ya mambo ambayo ni vyema ukajiepusha nayo kwa sababu yanaweza kukufanya ukajikuta uko katika wakati ambao haukuutarajia.

1. Hasira

Punguza sana tabia ya kuwa mtu wa hasira hasira, unayekasirika bila sababu za msingi. Jambo dogo tu umepandisha mori, utajikuta umefanya jambo ambalo litakugharimu.

Kumbuka, ni nadra kufanya maamuzi ya busara ukiwa na hasira. Rafiki mkubwa wa hasira ni matusi, ugomvi na mambo mengine yanayoambatana na ukosefu wa staha.

Katika nyakati hizi ngumu kimaisha, watu hawakawii kutumia udhaifu wa hasira zako kujinufaisha na ulichokifanya ulipokuwa na hizo hasira zako.

Watu watakupeleka polisi, serikali ya mtaa au hata kwa mjumbe wa nyumba kumi, ambako utajikuta ukilazimika kuingia mfukoni kwa jambo ambalo ungeweza kulishinda kwa kumezea tu.

Kuna watu wana maisha angalau kidogo ni mazuri, lakini wana hasira. Inapotokea hivyo wana kawaida ya kutoa maneno ya shombo, matusi au hata kurusha ngumi. Ni vyema ukatambua kwamba maneno ya kejeli kwa mwenzako, matusi au kumpiga, vyote ni kinyume cha sheria na unaweza kuadhibiwa hadi kifungo.

Kuna watu wanakuonea wivu na maisha yako lakini hawajui watakupataje. Wengine wanasubiri ujihukumu kwa udhaifu wako.

 

2. Jifunze kuwa peke yako

Nyakati hizi ni ngumu hivyo ina mambo mengi. Wapo baadhi yetu tuna kawaida ya kupitia labda baa kupata moja mbili kabla ya kurejea nyumbani. Katika kipindi hiki, ni vyema ukajifunza kuwa peke yako, hata kama ni baa.

Hii haimaanishi kuwa hautaki ushirikiano na wenzako, la hasha. Wape hi washkaji ukiwakuta, kisha sogea pembeni kwa sababu zozote, kama vile kuna simu muhimu naisubiri na kadhalika.

Hiyo ni kama ni lazima uende bar, lakini kama ishu ni kunywa, chukua vinywaji nenda kanywee nyumbani. Mwingine anaweza kusema hawezi kubeba bia kumi, fine, kuna bar karibu na unapoishi.

Ukifika mtume kijana akuchukulie bia zako nywea nyumbani kwako. Hii siyo tu itakupunguzia wadowezi, lakini itakuepusha na mambo mengi.

Nitakupa mfano halisi. Jamaa yangu mmoja alijikuta akikabiliwa na tuhuma ambazo hakuwahi kujua zilikotokea. Alitoka katika mihangaiko yake akafikia baa akisema apoze koo kidogo. Mara wakatokea vijana wawili na kujiunga naye.

Kwanza walimuagizia anachokunywa na baadaye akawanunulia nao pia. Wakajikuta wamekuwa marafiki kiasi cha hata kugongesheana mikono katika maongezi.

Ghafla wakatokea watu waliojitambulisha kama askari, wakawaambia wako chini ya ulinzi. Wakabebwa hadi kituo kimoja kidogo cha polisi ambako wale jamaa wawili walikiri kuwa ni wahalifu na kwamba huyo jamaa ni mwenzao!

Ule ulikuwa ni mchongo wa polisi na wale vijana, ikabidi jamaa yangu atoe fedha nyingi kunusuru mashtaka ambayo yangeweza kumpotezea gerezani. Mifano ipo mingi. Watu wanaweza kukujumuisha kwenye genge la uhalifu bila wewe kujua kuwa ulikuwa ni mchongo, lakini ukiwa na tabia ya kutojichanganya, unaweza kuepuka baadhi ya mambo.

No comments