Salaam za rambirambi zamiminika Tanzania

 


 

Kufuatia kifo cha Rais John Pombe Magufuli kilichotangazwa jana Machi 17, 2021, salam za rambirambi zimetumwa kutoka kwa viongozi na wasanii mbalimbali duniani.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson aliandika katika ukurasa wake wa Twitter, akielezea masikitiko yake kufuatia kifo cha Rais Magufuli.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi ametoa salamu za pole kwa taifa la Tanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Rais wa Somalia Mohamed Farmaajo ametoa salamu za pole kwa Tanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.

Kwa niaba yangu na kwa niaba ya Serikali na taifa la Somalia, ningependa kuwasilisha rambi rambi zetu kwa Jamhuri ya Muungano wa #Tanzania kwa kumpoteza Kiongozi Rais John Magufuli. Tunalitakia taifa Zima na Serikali subra na utulivu katika kipindi hiki cha maombi na maombolezo. pic.twitter.com/cQz3rALaPt

— Mohamed Farmaajo (@M_Farmaajo) March 17, 2021

Rais wa Venezuela Nicolás Maduro ametoa salamu za pole kwa Tanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Kosovo Behgjet Pacolli ametoa salamu kwa Tanzania kufuatia kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 majira ya saa 12:00 Jioni.

Mama Samia amesema Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli amefariki kwa maradhi ya moyo katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Licha ya viongozi hao wa kisiasa, pia wasanii mbalimbali, wakiongozwa na Bob Wine wa Uganda, nao walituma salamu zao za pole kufuatia msiba huo mkubwa. Nyota wa muziki wa Uganda pia, Jose Chamilion naye alituma salamu za pole kwa watanzania kwa msiba huo mzito.

Nyota namba moja wa Bongo Flava nchini, Diamond Platnumz alituma salam za pole kwa familia, Makamu wa Rais na watanzania wote juu ya msiba huo, kama alivyofanya Vanesa Mdee, Shilole na wengineo kadhaa.

Related ArticlesLiLi

No comments