Simba ndiyo imemponza Cedric Kaze
Benchi la mfundi la klabu ya Yanga limefumuliwa. Mengwa mkuu ni Cedric Kaze, aliyekuwa Kocha Mkuu.
Wenye timu yao wamesema matokeo ndiyo chanzo cha kufukuza benchi hilo, lakini wenye kuuelewa mpira wa Tanzania, wanakuambia soka safi la Simba ndiyo chanzo cha vurugu mechi huko Jangwani.
Viongozi na mashabiki wa Yanga, pamoja na kutaka ushindi kwa timu yao inayoongoza Ligi kwa muda mrefu, pia wanataka soka la kuvutia uwanjani. Ndiyo maana walimfuata Kaze, Mburundi aliyekuwa akifanya kazi ya kufundisha soka katika academy ya Barcelona, iliyopo kule Canada.
Yanga waliamini, kwa kuwa Kaze anafundisha watoto wenye falsafa ya kutandaza soka la pasi nyingi, basi angeweza kuileta falsafa hiyo na kufanyaq kazi.
Lakinj kwa muda wote ambao ameifanya kazi hiyo pale Jangwani, Kaze ameshindwa kuleta mabadiliko ya Yanga uwanjani. Pengine hilo lisingekuwa tatizo kama mahasimu wao wakubwa Simba wangekuwa nao hawafanyi vizuri. Lakini tatizo Simba wanaonekana kuwa na kiwango kizuri uwanjani, wakicheza soka la pasi na kutishia kwa kiwango kikubwa nafasi yao.
Simba licha ya kuwa hawaongozi Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini kwa michezo minne iliyotanguliwa na Yanga, ikishinda yote, jamboi ambalo linawezekana kwa Simba hii, itakuwa mbele kwa pointi saba mbele ya Yanga, kitu ambacho mashabiki wa wananchi hawakipendi abadan.

Post a Comment