ERIKALI YAANZA UJENZI WA RELI YA KISASA KIPANDE CHA MWANZA- ISAKA
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainab Telack akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Shirika la Reli Nchini Bw. Masanja Kadosa wa kwanza kushoto walipofika eneo la Bandari Kavu ya Isaka ili kujionea namna gani upanuzi wa bandari hiyo utakavyoleta ufanisi wa biashara na uwekezaji katika mikoa ya kanda ya Ziwa, Wengine katika Picha ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Yasinta Mboneko na Katibu Tawala Mkoa Shinyanga Bw. Albert Msovela
Na Anthony Ishengoma
Serikali imeanza ujenzi wa
kipande cha Reli ya kisasa ya SGR kwa kipande cha Isaka-Mwanza chenye thamani
ya Dora za Kimarekani Bil.1 mradi ambao utakuwa wa na manufaa makubwa kwa Nchi
jilani za Uganda, Rwanda na Burundi pamoja na mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Akiongea wakati wa kutambulisha
ujenzi wa mradi Mkurugenzi wa Shirika la Reli nchini Masanja Kadogosa alitaja
faida za mradi huo kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa kuwa utarahisisha usafiri kwa
wakazi hao kwenda Dodoma na Dar es salaam lakini pia Bandari Kavu ya Isaka
itatumika kupokea na kushusha mizigo yote ya Nchi jilani.
Bw. Kadogosa aliongeza kuwa
ujenzi wa reli hii ya kisasa utaenda sambamba na upanuzi wa Bandari kavu ya
Isaka kwa lengo la kuiongezea ufanisi kwa kuhakikisha Nchi za jirani
zitakapoagiza mizigo ziwe zinapokelea mizigo yake Isaka moja kwa moja tofauti
na sasa ambapo mizigo inafuatwa Dar es Salaam.
Aidha Bw. Kadogosa alisema pamoja
na kuwepo kwa faida hizo lakini pia shughuli za ujenzi wa reli hiyo ni fursa
kubwa kwa wakazi wa Shinyanga kwani watapata ajira na ujuzi kwa kushiriki
katika mradi huu mkubwa utakaoa chukua miezi 36 mpaka kukamilika kwake.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga
Bi. Zainab Telack akiongea katika bandari kavu ya Isaka alitaka ujenzi wa reli
hiyo kuzingatia na kujenga kipande cha reli kuelekea eneo la viwanda lililopo
Manispaa ya Kahama na kuongeza kuwa upanuzi wa Bandari Kavu ya Isaka utavutia
zaidi wawekezaji ambapo tayari wawekezaji katika saruji na kiwanda cha nguo
wako tayari hivyo upanuzi wa bandari hiyo ni muhimu kwa wawekezaji wa mkoa huo.
Aidha Bi. Telack alihaidi kutoa
ushirikiano katika nyanja zote zinatakiwa kufanyiwa kazi ikiwemo kuwa andaa
wananchi kupokea mradi huo lakini pia kushirikiana na shirika la reli kutatua
changamoto zitakazojitokeza ikiwemo suala la ardhi na kuhamisha baadhi ya
miundombinu itakayoingiliana na ujenzi huo.
Aidha diwani wa Kata ya Isaka Bw.
Pazi Majuto Pazi aliongeza kuwa ujenzi wa Reli mpya na ya Kisasa ni fursa kwa
wakazi wa Isaka kujipatia Ajira katika mradi wa ujenzi lakini akawa na wasiwasi
na baadhi ya wageni ambao tayari wako Isaka kusaka ajira hiyo kuwa wanaweza
kuwakosesha fursa wakazi wa eneo lake la utawala.
Ujenzi wa reli ya kisasa ni
mwendelezo wa ujenzi wa reli hiyo hapa Nchini ambao tayari
inaendelea kwa kipande cha Dar es Salaam-Morogoro na Morogoro- Makutopola
Singida.
.

Post a Comment