Burna Boy, Wizkid washinda Grammy
Wasanii maarufu wa Nigeria Burna Boy na
Wizkid wameshinda tuzo za Grammy za mwaka huu wa 2021.
Burna Boy ameshinda tuzo ya kipengele cha kuwa na Albamu bora ya muziki wakati
Wizkid ameshinda katika kuwa na video bora zaidi kwa wimbo wake aliomshirikisha
Beyoncé unaoitwa Brown Skin Girl, kutoka Lion King: Albamu ya The Gift.
Binti yake Beyoncé Blue Ivy alikuwa mshindi katika wimbo huo huo.
Katika kipengele cha video bora, tuzo inatolewa kwa msanii, muongozaji wa video
na muandaaji wa video pia.
Burna Boy, ambaye jina lake halisi ni Damini Ogulu, ambaye ameshiriki kwa mwaka
wa pili ameshinda katika albamu yake ya Twice As Tall .
Tuzo ya Grammy ya 63 imefanyika mjini Los Angeles. Kwa kawaida huwa sherehe
kubwa ya muziki ikifanyika kila mwaka lakini mwaka huu hali imekuwa tofauti
kutokana na janga la corona.
Hakuna watazamaji, na watumbuizaji walikuwa wametengwa katika majukwaa matano,
na wakiwa kwa umbali.
Burna Boy, mwenye miaka 29, amewashinda wengine wanne ikiwemo bendi ya Malian,
Tinariwen.
Tuzo za Grammy zimeielezea albamu ya Twice As Tall kuwa muziki uliotengenezwa
kwa kiwango cha juu cha kimataifa, ni fundisho kuwa pia kwa wegine na ndio
maana imemfanya Burna Boy kuingia katika kiwango hicho cha kimataifa".
Aliendelea kusema kuwa albam hiyo imechanganya miondoko mbalimbali kama midundo
ya pop, Afrobeat, dancehall, reggae na miondoko mingine mingi.
Albumu yake ilishirikisha wanamuziki wengi duniani wakiwemo Stormzy, Youssou
Ndour, Naughty By Nature, na Chris Martin wa Coldplay, na vilevile Sean Combs
akiwa muandaaji mkuu.
Video ambayo imemfanya Wizkid kushinda imeelezewa kuwa imezingatia mitindo na
kusheherekea urembo wa mwanamke mweusi mahali popote duniani.
Burna Boy amechaguliwa katika kipengele kilekile cha mwaka 2019 -
kinachojulikana kama 'Best World Music Album' - lakini Angelique Kidjo alishinda
katika tuzo za mwaka 2020.
Ingawa Kidjo aliamua kutoa ushindi wake kwa Burna Boy, alisema: "Burna Boy
ni miongoni mwa wasanii wachanga ambao wanatoka Afrika ambao wanabadili mtazamo
wa muziki wa Afrika."
Mwanamuziki huyu aliyezaliwa Nigeria, Burna Boy alizindua albamu yake ya kwanza
ya LIFE, mwaka 2013.
Na baadae alizindua albamu ya Redemption mwaka 2015 na Outside mwaka 2018
ambayo ilijumuisha ngoma iliyovuma kimataifa
Lakini ilikuwa katika albamu yake ya mwaka 2019 ya African Giant ambapo Burna
Boy alijulikana zaidi kimataifa na kupata tuzo yake ya kwanza ya Grammys.
Akiwa analinganishwa na mwanamuziki wa Nigeria Fela Ransome-Kuti na kupata
umaarufu barani Afrika.
Wakati wa mgogoro wa ubaguzi Afrika Kusini mwaka 2019, alitishia kutoenda
katika taifa hilo kama serikali ya nchi hiyo haitachukua hatua dhidi ya
xenophobic.
Pia alijumuishwa katika maandamano ya #EndSARS ya kupinga unyanyasaji wa
polisi, alitoa wimbo wa wahanga ambao waliuawa katika maandamano hayo Oktoba
20,2020 katika geti la Lekki Toll Gate mjini Lagos.
Vilevile ameandika katika kurasa yake ya tweeter kuunga mkono waandamanaji wa
Senegal ambao walijitokeza barabarani baada ya kiongozi wa upinzani Ousmane
Sonko kukamatwa.
BBC/SWAHILI

Post a Comment